RAIS
Jakaya Kikwete ameagiza kero za madereva nchini, zianze kutatuliwa na
ripoti za hatua zitakazoanza kuchukuliwa kuanzia kesho, zipelekwe kwake
moja kwa moja.
Amesema
hayo jana alipokutana na wanachama wa Chama kipya cha Madereva (TADWU),
wakati alipokutana nao jijini Dar es Salaam akiwa na maofisa wa Wizara
ya Kazi na Ajira, Kikosi cha Usalama Barabarani na Mdhibiti wa Usafiri
wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra).
Akizungumza
katika mkutano huo baada ya kupokea risala ya madereva hao, Rais
Kikwete aliagiza Sumatra kumpa taarifa ya namna walivyojipanga kukagua
madereva wenye mikataba na wasio na mikataba.
"Jumatatu
lazima mnipe taarifa ya mkutano wenu, Sumatra kwenye hiyo mikataba
mnahakiki nini na nani ana mkataba na nani hana mkataba," alisema Rais Kikwete.
Rais
Kikwete aliwataka Sumatra pia kusimamia mazungumzo kati ya wamiliki wa
magari na madereva na kupata muafaka katika matatizo ambayo yamekuwa
yakilalamikiwa na madereva hao kwa muda mrefu bila ufumbuzi hasa katika
masuala ya posho na mishahara.
"Mikataba
ambayo inaonesha mtu analipwa kiasi gani na posho yake ni kiasi gani
hiyo ndiyo mikataba kamili, hata mimi nilipoingia, nilipewa mkataba
unaoeleza kwa miaka mitano Rais unastahili hiki na hiki," alisema Rais Kikwete.
Rais
Kikwete alisema hana mamlaka ya kupanga posho lakini aliwataka Sumatra
kukaa chini na wamiliki wa magari, madereva na Wizara ya Kazi na Ajira
kupanga namna ya kuwalipa madereva.
"Mnapotegemewa kusimamia na hamsimamii vizuri mnatengeneza manung'uniko... tendeni haki, simamieni vizuri," alisema Rais Kikwete.
Awali
Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Giliad Ngewe aliwekwa katika wakati mgumu
na Rais Kikwete baada ya kuulizwa maswali ni lini wanapitia mikataba ya
madereva hao, ambapo alijibu kwa kusua sua jambo lililofanya madereva
waliojaa katika ukumbi huo kumzomea.
Rais
Kikwete alibaini kuwa madereva wengi hawana mikataba jambo
lililosababisha wafanye kazi katika mazingira magumu ambapo aliwataka
Sumatra kuhakikisha madereva wote wana mikataba.
Alisema sekta ya usafirishaji inachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi na madereva ndio wanaoendesha uchumi wa nchi.
Alisema sekta ya usafirishaji inachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi na madereva ndio wanaoendesha uchumi wa nchi.
Kuhusu
madai ya madereva kupigwa tochi na askari wa usalama barabarani wawapo
safarini, aliwataka madereva hao kutii sheria sambamba na kuzingatia
sheria za usalama barabarani.
Alisema
madereva nao wamekuwa wakikiuka sheria za barabarani na kusababisha
ajali nyingi zinazotokea nchini na kusababisha maafa makubwa na upotevu
wa mali.
Rais Kikwete alitoa mfano wa alama za barabarani zinazoonesha kuwa dereva hapaswi kwenda kwa kasi ya zaidi ya kilometa 80 kwa saa, lakini unakuta dereva ndio anakanyagia kasi ya kilometa 120 kwa saa.
Rais Kikwete alitoa mfano wa alama za barabarani zinazoonesha kuwa dereva hapaswi kwenda kwa kasi ya zaidi ya kilometa 80 kwa saa, lakini unakuta dereva ndio anakanyagia kasi ya kilometa 120 kwa saa.
Alisema
kama madereva wangekuwa wakitii sheria na alama za barabarani,
kusingekuwa na haja ya hizo tochi, lakini vifaa hivyo vinawekwa kutokana
na madereva kutotii sheria.
Mbali
na hayo, Rais Kikwete pia aligusia suala la kuzidisha mizigo katika
magari na kusema madereva wamekuwa wakipewa uzito maalumu wa mizigo yao,
lakini wanazidisha, hata hivyo madereva hao walipiga kelele kuwa ni
tatizo la wamiliki.
Mpinga na Matrafiki
Hata hivyo, alimtaka Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, kuondoa matrafiki wanaoomba rushwa barabarani.
Alisema
madereva wa nje ya nchi wanaobeba mizigo kutoka Bandari ya Dar es
Salaam kwenda katika nchi zao, wamewaeleza viongozi wao kuwa wamekuwa
wakilazimika kuwa na bajeti ya rushwa wanazoombwa na trafiki
barabarani.
Aliwapongeza madereva kwa kuanzisha chama cha kuweka na kukopa na kusema kuwa naye atawasaidia.
Kuhusu
mafunzo, alimuagiza Kamanda Mpinga kutafuta namna ya kuzungumza na
wamiliki wa magari, ili mafunzo hayo ya kila baada ya miaka mitatu,
yafanyike kwa utaratibu utakaotunza ajira za madereva na gharama zilipwe
na wamiliki.


Note: Only a member of this blog may post a comment.