Ukitaka kujua muziki mzuri unaokubalika mitaani kuna sehemu za kupita alafu unatoka na majibu kamili kabisa, moja ya sehemu hizo ni Club.. ukikatisha Club sio rahisi kukuta DJ kapiga midundo yote kwenye playlist alafu akaiacha ngoma ya AMARULA ambayo imeimbwa na mkali kutoka Zambia, Roberto.
Niliipata story kwamba jamaa anatua Mwanza, nikaona hata nisipitwe !! Kuna sababu zote kumshuhudia huyu mkali kutoka Zambia.. Kingine ni kwamba katika nchi ambazo zinafanya poa na tunasikiliza muziki wake, majina ya Wasanii toka Zambia hayasikiki kwa uzito mkubwa kama ilivyo kwa South Africa, Tanzania, Kenya, Uganda, Nigeria na nchi nyingine.
Nimeishuhudia show ya kwanza ya Roberto ndani ya TZ +255 ambayo imefanyika Jijini Mwanza, Jembe Beach… ilikuwa burudani kwa watu wa nguvu wa Rock City Mwanza.
Friends wakiongozwa na Boss wa Jembe Sebastian Ndege kwenye picha na Roberto.
DJ K-flip wa Jembe FM kwenye kazi yake mwanzo mwisho !!
Roberto akaitawala stage ya Jembe Beach.. Burudani ikaanza na kuendelea.
Warembo wakasogea pia kumpa tafu Roberto ili kuongeza burudani zaidi.

Note: Only a member of this blog may post a comment.