Mayasa mariwata
ULE mjengo wa staa wa filamu Bongo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ ambao alimzawadia mama yake Lucresia Karugila, imedaiwa
umeshindikana kuuzika baada ya kutangaza kuupiga bei ya shilingi milioni
hamsini.
Mjengo wa staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Lulu na mama yake walifikia uamuzi wa
kuupiga bei mjengo huo uliopo maeneo ya Kimara Saranga jijini Dar baada
ya kuona mazingira ya eneo hilo si mazuri hususan kipindi cha mvua
kutofikika kwa urahisi.“Wamedhamiria kuipiga bei nyumba hiyo lakini wanashindwana na wateja kutokana na pesa hiyo ndefu anayoitaka wakati kiuhalisia nyumba haina hadhi.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Kutokana na ishu hiyo paparazi wetu alimtafuta Lulu ambaye simu yake
iliita bila kupokelewa lakini mama Lulu alipotafutwa kuzungumzia ishu
hiyo alisema:“Hii nyumba ni yetu hata kama tukiiuza kwani kuna tatizo gani sioni kama kuna cha ajabu hapo mpaka mkae mnatufuatilia kiasi hicho, nimeshasema hayo ni mambo yetu binafsi hayawahusu sababu hamkutusaidia kujenga, nimetoka msibani bado nina majonzi sitaki kuongelea tena hayo mamboº.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.