Monday, September 7, 2015

Anonymous

VIDEO&PICHAZ: Didier DROGBA Adhihirisha Ubora Wake Ligi Kuu Marekani...Shuhudia Alivyowaduwaza Watu Hapa!

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ivory Coast Didier Drogba, ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Montreal Impact inyoshiriki Ligi Kuu Marekani (MLS), ameanza vizuri katika mechi yake ya kwanza toka ajiunge na Ligi hiyo.
2C030EF500000578-3223977-image-a-39_1441523066870
Drogba aliyejiunga na timu hiyo kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Chelsea, alifanikiwa kuifungia timu hiyo goli 3 (hat-trick) katika ushindi wa goli 4-3 dhidi ya klabu ya Chicago Fire. Huo ni mwanzo mzuri kwa staa huyo wa Afrika katika Ligi Kuu Marekani.
2C030F2C00000578-3223977-image-a-38_1441523015210
Video ya magoli yote pamoja na Hat-trick ya Didier Drogba nimekuwekea hapo chini

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.