Akiwahutubia
wananchi hao katika mkutano wake wa kampeni kwenye mji wa Kiomboi Jimbo
la Iramba Magharibi, mkoani Singida akiwa katika siku yake ya mwisho
mkoani hapa, alisema mafisadi hao wakifanikiwa kununua kadi hizo
hawatashindwa kuwauza wenyewe iwapo watachaguliwa kuingia Ikulu.
Aliwatahadharisha
wananchi wasikubali ulaghai kwa kuwa kufanya hivyo ni kuuza haki yao ya
msingi ya kumchagua kiongozi wanayemtaka.Pia aliwataka mawakala
wake wasikubali kulaghaiwa ili wabadili matokeo.
“Tuna
taarifa kwamba wameanza kuweka mipango ya kununua kadi za kupigia kura,
msikubali ulaghai huo maana watu hao wakichaguliwa ni hatari kwa nchi,
kama watanunua kadi zenu watashindwaje kuwauza nyinyi wakiingia Ikulu?” Alihoji.
Akiwa
katika jimbo la Iramba Mashariki, Dk. Magufuli alimrushia kijembe
aliyekuwa Mbunge wa Iramba Mashariki kwa tiketi ya chama hicho, kuwa
alichelewesha maendeleo ya jimbo hilo.
Huku
akimnadi mgombea wa jimbo hilo ambalo kwa sasa linaitwa Mkalama, Allan
Kiula, alisema mbunge huyo aliliongoza jimbo hilo kuanzia mwaka 1995
hadi 2010 alipoangushwa kwenye kura za maoni na sasa anagombea Jimbo la
Singida Mjini kwa tiketi ya Chadema.
Akizungumza
bila kumtaja jina, Dk. Magufuli alisema mbunge huyo amekaa muda mrefu
lakini hakuna lolote alilowachia wananchi kwani alikuwa mpiga porojo.
“Mlikosea kuchagua mbunge hapa Iramba, mbunge wenu
alikaaa muda mrefu lakini amewachelewesha, yeye alikuwa mtu wa porojo
tu na ndiyo maana hivi sasa ameamua kuwakimbia na kwenda kugombea jimbo
lingine kwasababu anajua angeanguka huku,” alisema Dk. Magufuli na kuongeza.
“Hivi
niwaulize ukiwa na paka nyumbani kwako akakimbilia porini si anabaki
kuwa paka tu, sasa msifanye makosa nichagulieni Allan maana namjua kwa
uchapakazi wake,” alisema.
Dk.
Magufuli aliahidi kujenga nyumba za watumishi kwa ajili ya wilaya mpya
ya Mkalama ili wafanyakazi wote wanaoajiriwa waishi karibu na makazi ya
wananchi.
Alisema
akiwa rais ataagiza kujengwa kwa nyumba za walimu ili iwe motisha kwa
walimu wanaoajiriwa kufanyakazi katika Wilaya hiyo ya Mkalama.
Mgombea
huyo aliwaomba wananchi wa vyama vyote vya siasa kumpa kura akiahidi
kuwa atakapochaguliwa atakuwa rais wa Watanzania wote bila kubagua vyama
vyao.
“Chadema
mnasema people’s power, sasa hiyo power msikae nayo bure nipeni mimi
Magufuli hiyo power niingie Ikulu nikawafunge mafisadi kwa makufuli
yangu,” alisema Dk. Magufuli na kuamsha shangwe kwa wananchi waliokuwa wakimsikiliza.


Note: Only a member of this blog may post a comment.