Friday, August 28, 2015

Anonymous

Mgombea Mwenza Kumwangusha John MAGUFULI Urais 2015

Kuna sababu 3 zitakazopelekea CCM ianguke kwa kuwa na mgombea mwenza mwanamke:
1. Mfumo dume bado una nguvu katika makabila mengi hususani vijijini. Wananchi wengi hawaamini kama wanaweza kuongozwa na rais mwanamke hivyo kumnyima kura.

2. Kushindwa kwa Bi.Anne Makinda katika kulisimamia bunge lililopita ambalo lilitawaliwa na ubabe na kubebwa CCM. Ni katika bunge hili wananchi wameshuhudia sheria mbalimbali za hovyo zikipitishwa kibabe na serikali chini ya ulinzi mkali wa spika Anne.

3. Mgombea mwenza ndiye alikuwa makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba; chini ya usimamizi wake tulishuhudia kanuni zikivunjwa ili kuichakachua katiba ya wananchi.

Ni katika kipindi hicho tulishuhudia matusi, kejeli, na vitimbi kutoka kwa wajumbe, huku wakitetewa na uongozi wao. Na kutokana na uchakachuaji huo ndipo ukawa ilizaliwa rasmi chini ya mgombea huyu.
Leo hii anaenda kwa wananchi waliotoa maoni ya katiba kutaka achaguliwe urais...ccm na Magufuli mnalo mwaka huu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.