Thursday, September 10, 2015

Anonymous

MSUVA wa YANGA SC Achimba MKWARA Mzito!

Msuva..[1]

Mfungaji bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara, Simon Msuva.
Wilbert Molandi, Dar es Salaam
MFUNGAJI bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara, Simon Msuva, amekuja juu na kutamka kuwa, wale wanaomwambia makali yake yameisha, basi wasubirie Ligi Kuu Bara ianze.
Nyota huyo anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji, msimu uliopita alimaliza ligi kuu akiwa mfungaji bora kwa kupachika mabao 17, akifuatiwa na mshambuliaji wa timu hiyo, Amissi Tambwe, aliyefunga 14. 

Msuva ameonekana kupungua makali yake baada ya kufanikiwa kufunga bao moja tu ndani ya michezo12 aliyocheza mpaka sasa.
Akizungumza na Championi Jumatano, Msuva alisema anaamini kuwa, kikubwa yeye akili na nguvu zake zote alizielekeza kwenye ligi kuu, hivyo hata kitendo cha kushindwa kufunga kwenye mechi za Kombe la Kagame na kirafiki hakimuumizi kichwa kabisa.
Msuva alisema, kikubwa yeye amejipanga katika kutetea kiatu cha dhahabu anachokishikilia ili kuendeleza rekodi yake. 

Aliongeza kuwa, anaamini msimu ujao wa ligi kuu ushindani utaongezeka kwa kiasi kikubwa, lakini kama mshambuliaji amejipanga kuhakikisha anakabiliana nao.
“Wanaosema uwezo wangu wa kufunga umepungua, wasubiri ligi kuu ianze halafu waone uwezo wangu ndani ya uwanja.
“Mimi akili na nguvu zangu zote nimezielekeza  zaidi kwenye ligi kuu na siyo kwenye Kagame na mechi za kirafiki tulizocheza ambazo nilifunga bao moja pekee dhidi ya Kimondo,” alisema Msuva.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.