MAGEUZI! Mama mzazi wa staa wa filamu za Bongo,
Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila ametoa baraka kwa bintiye
huyo ambaye kiimani ni Mkristo, kufunga ndoa ya Kiislam kwa madai kuwa
ndoa si dini bali ni utu wa mtu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kuna barua za posa mbili ambazo mwanamke huyo mwenye misimamo amekuwa akizikataa kutokana na wahusika kuwa na imani tofauti na Lulu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, kuna barua za posa mbili ambazo mwanamke huyo mwenye misimamo amekuwa akizikataa kutokana na wahusika kuwa na imani tofauti na Lulu.
Staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa na mamaake.
CHANZO CHAANIKA MSIMAMO WA MAMA LULU
“Unajua mama Lulu ni mwanamke mwenye misimamo sana. Akishikilia jambo
kashikilia. Posa mbili zilishafika akagoma katakata, kisa waoaji si
Wakrsito. Lakini hilo nalo limeonekana kumuumiza kisaikolojia Lulu maana
hajui ni mwanaume gani aliyepangiwa na Mungu.
“Watu wengi wamekuwa wakimlaumu sana mama Lulu wakidai kuwa anakataa
posa za wanaume wa Kiislam kwa kigezo cha dini lakini kumbe anataka tu
akae na mwanaye pale nyumbani.”
“Ninavyojua mimi, kikubwa kilichokuwa kikimfanya mwanamke huyo
ashikilie msimamo huo ni historia yake. Anasema katika ukoo wake na wa
baba Lulu (Michael Kimemeta) hakuna Muislam (mwanaume) aliyeoa hapo wala
Mkristo (mwanamke) aliyekwenda kuolewa na Muislam,” kilisema chanzo.
...Baba Lulu.
MAHOJIANO
Amani lilimuuliza kama miongoni mwa wachumba wawili waliojitokeza
kumchumbia Lulu wakakataliwa, yupo staa wa sinema za Bongo, Mahsein
Awadhi ‘Dk. Cheni’ ambaye hivi karibuni aliripotiwa na gazeti ndugu na
hili (Ijumaa) kuwa siku hizi yupo ‘vere klozdi’ na Lulu, mahaba
yakatajwa, lakini alitoa majibu ya njia panda bila kusema ni kweli au
kinyume chake!
Chanzo: “Sina hakika. Ila wapo wawili. Nadhani mama Lulu mwenyewe
anajua. Nendeni mkazungumze naye. Ila ni mtata sana yule mama, si wa
kumwingia kirahisirahisi tu.”
Amani: “Kwani Lulu mwenyewe alikuwa tayari kuolewa Kiislam?”
Chanzo: “Inasemekana yeye yuko tayari.”
Chanzo: “Inasemekana yeye yuko tayari.”
KUHUSU BABA LULU
Amani lilimuuliza mtoa habari huyo kama anajua msimamo wa baba Lulu
kuhusu mwanaye kubadili au kutobadili imani.Chanzo: “Unajua yule mzee
ana maisha yake kwa sasa. Ana familia yake. Lulu ni mwanaye lakini
naamini mwongozo mkubwa anaupata huku Dar kwa mzazi mwenzake (mama
Lulu).”
Dk. Cheni.
MAMA LULU ASAKWA
Juzi, Amani lilimsaka mama’ke Lulu na kufanikiwa kumpata kwa njia ya
simu ambapo mahojiano yake na paparazi wetu yalikuwa kama ifuatavyo:
“Labda niseme kwanza mimi mtoto wangu hajawahi kuletewa posa nyumbani, isitoshe hata yeye mwenyewe hajawahi kuniletea mchumba na kuniambia kuwa anataka kumuoa.
“Labda niseme kwanza mimi mtoto wangu hajawahi kuletewa posa nyumbani, isitoshe hata yeye mwenyewe hajawahi kuniletea mchumba na kuniambia kuwa anataka kumuoa.
“Awali nilipenda mtoto wangu aolewe na mtu wa imani yake kwa sababu
yeye mwenyewe amekulia katika Ukristo mpaka kufikia hapa alipo
sasa.“Lakini siku hizi wazazi wanaangalia utu wa mtu na vitu vingine
vinakuja baadaye kabisa, kwa vile anaweza hata akaolewa na mwanaume wa
dini yake bado akamletea shida maishani.
“Ngoja nikwambie, kwanza
sidhani kama sasa hivi mapenzi yanaangalia dini wala kabila. Kama yeye
atamleta Muislam na kampenda kutoka kwenye moyo wake na mimi nitampokea
wala sitakuwa na pingamizi lolote.
AMANI LARUDI KWA DK. CHENI
Baada ya Amani kumalizana na mama Lulu, lilirudi kwa Dk. Cheni
anayetajwa hivi karibuni ‘kutoka’ na Lulu ambapo aliulizwa kwa staili
kuwa, wasomaji wa gazeti hili wanataka kujua kama kweli atamuoa Lulu.
Alijibu:
“Hebu kaeni chini mtafakari nchi ya Japan wanatengeneza magari lakini nyie hata baiskeli hamuwezi. Tafakarini ubunifu wenu siyo mambo ya watu.”
Amani lilimkosa Lulu hewani lakini maelezo ya mama yake kama mkuu wa
familia yalitoa picha ya msimamo kuhusu binti huyo ambaye hivi karibuni
aliripotiwa kujikita kwenye maombi kwa kusali na kumwabudu Mungu katika
roho na kweli japo mara kadhaa amewahi kunaswa akipombeka kama ishara ya
shetani kumzidi mabavu.
Note: Only a member of this blog may post a comment.