Mambo Matano MAKUBWA Yanayosaidia Kukuza Taaluma Yako
Kwanini kukua kwako na kuendelea kunahitajika sana? Ni muhimu katika
kuleta changamoto na wewe mwenyewe kujiongeza zaidi na wala usilete
maneno ya kuwa umetingwa na kazi zaidi sehemu ambayo huwezi kukua na
kujifunza zaidi.
Kuna uwezo kwa kila mtu zaidi ya vile tunavyoona na kujua, hivyo ni
muhimu kwa kila mmoja wetu kukua na kuongezeka binafsi na taaluma yake
pia. Hii si tu ili upate kazi bora zaidi lakini pia inakufanya ufanye
kazi kwa ufanisi na kujitosheleza zaidi. Hapa kuna mambo matano ambayo
unaweza kuyafanya binafsi bila msaada ya kampuni au shirika unalofanyia
kazi,
1. Chukua changamoto mpya
Hii inaweza kuwa hatari kwa wakati mwingine na kuchanganya wakati
mwingine ingawa inategemea na shirika na kampuni uliyopo. Wakati
mwingine changamoto huonekana kujitokeza mara kwa mara wakati hujamaliza
ile ya kwanza lakini hiyo inaonyesha unakua na kukamaaa hivyo fursa
zikijitokeza utakuwa wa kwanza kuzikumbatia.
- Soma.
Unahitaji kusoma sana na si tu masomo ya darasani bali majarida mengi
yanayohusiana na taaluma yako na vitabu vyenye tafiti mbalimbali
inasaidia kukuongeza ufahamu zaidi wa mambo mengi kwenye taaluma yako na
kuwa na wigo mpana katika kushughulikia matatizo.
- Wekeza katika kujifunza
Kuna masomo mengi yanatolewa bure kwenye mitandao mbalimbali, tenga muda wako ili uweze kujiongezea ufahamu kwa njia ya mtandao.
- Pata mkufunzi wako
Hebu tafuta katika shirika hilo unalofanyia kazi na uone kama kuna
mtu ambaye anaweza kuwa mkufunzi wako wa mambo ya taaluma. Kama hakuna
tafuta nje ya taasisi hiyo kwa mtu mwenye uelewa zaidi kuliko wewe na
mwenye haiba ambayo unaweza kujifunza kutokakana na maisha yake na
taaluma yake pia. Ni muhimu kuwa na mawasiliano ya karibu na mtu ambaye
unataka kujifunza kwake.
- Jizingire na watu wenye uelewa na ufahamu kama wa kwako..
Hakikisha marafiki zao na watu wako wa karibu ni wenye uelewa kama wa
kwako na mitazamo yako ya kuendelea kukua na kujifunza. Watu wenye
akili ambazo hazina moyo wa kujifunza na kukua achana nao, hawatakuelewa
sasa lakini baadaye watakuelewa. Kila siku kuna fursa ya kujifunza na
kujiboresha katika fikra na utendaji wako kwenye taaluma yako. Hakuna
namna nyingine lazima tukue kutoka hapa tulipo na kuweza kufanya mambo
makubwa laini inaanzia kwenye fikra binafsi.
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Filed Under:
MAKALA
on Saturday, September 5, 2015
Note: Only a member of this blog may post a comment.