Thursday, September 10, 2015

Anonymous

ATHUMAN IDD 'CHUJI': Nimerejea Rasmi!

athumani iddi

Kiungo mkabaji wa zamani wa Yanga, Athumani Idd ‘Chuji’.
Wilbert Molandi, Dar es Salaam
KIUNGO mkabaji wa zamani wa Yanga, Athumani Idd ‘Chuji’, amepona maumivu yake ya nyama za paja na amerejea uwanjani kwa ajili ya kuichezea timu ya Mwadui FC ya Shinyanga.
Chuji, hivi karibuni alipata majeraha ya nyama za paja na kusababisha ashindwe kucheza baadhi ya mechi za kirafiki za kujiandaa na ligi kuu ikiwemo dhidi ya Simba na Azam FC.
Mkongwe huyo alikuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili, sawa na siku 14, akiuguza majeraha hayo baada ya kuumia mazoezini kabla ya kupatiwa matibabu. 

Akizungumza na Championi Jumatano, kiungo huyo alisema anafurahi kupona maumivu hayo na kurejea uwanjani kwa ajili ya kuuanza msimu mpya wa ligi kuu akiwa fiti kwa ajili ya mapambano.
Chuji alisema, kurejea kwake kutaboresha kikosi chao akitumia ukongwe wake kuisaidia timu hiyo inayoundwa na nyota wakubwa akiwemo Nizar Khalfani, Jabir Aziz, Shaaban Kado, Razak Khalfan na mkongwe Bakari Kigodeko. 

“Ninafurahi sana kupona nyama za paja huku ligi kuu ikitarajiwa kuanza Jumamosi ya wiki hii, hivi sasa nipo fiti kabisa kwa ajili ya mikikimikiki ya ligi kuu.
“Ninaamini uwepo wangu kwenye timu utakisaidia kikosi chetu cha Mwadui, hivyo nimemaliza programu ya mazoezi mepesi ya binafsi, hivi sasa ninafanya mazoezi magumu ya pamoja na wenzangu,” alisema Chuji.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.