Monday, September 7, 2015

Anonymous

Msenegali Mpya SIMBA SC Amtia Kiburi MGOSI

02-Msenegali Msenegali, Pape Abdoulaye N’daw.
Said Ally, Dar es Salaam BAADA ya uongozi wa Klabu ya Simba kufanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji Msenegali, Pape Abdoulaye N’daw, nahodha wa kikosi hicho, Mussa Hassan Mgosi, ametamka wazi kuwa anaamini muunganiko wao na mshambuliaji huyo utaweza kuisaidia timu hiyo kufanya vyema katika michezo yake ya ligi kuu msimu ujao.
Msenegali huyo amesajiliwa na Simba kwa dau linalofikia dola 10,000 (zaidi ya shilingi milioni 20) kwa mkataba wa mwaka mmoja.


Akizungumza na Championi Jumatatu, Mgosi alisema kuwa kutokana na jinsi alivyomuona straika huyo akicheza, anaamini atakuwa msaada mkubwa ndani ya timu yao katika eneo la ushambuliaji na atakuwa chachu mojawapo ya mafanikio yao.
“Ni jambo zuri kuona tupo na Pape N’daw katika kikosi chetu, kwani kwa jinsi ambavyo nimemuona, naona ana vitu fulani ambavyo atavitumia na vitakuwa msaada mkubwa sana kwetu, hasa kwa upande wa ushambuliaji.


“Naamini kwa muunganiko huu tulionao mimi, Kiiza na Pape na wengine, tutaweza kuwa mwiba kwa mabeki wa timu pinzani ambapo tunapenda kuwaambia wajiandae vya kutosha kuweza kutukabili kwani moto wetu utakuwa wa hali ya juu, lengo likiwa ni kutaka kufanya vyema,” alisema Mgosi.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.