Monday, September 7, 2015

Anonymous

MBEYA CITY Mpaka Kieleweke!

Martha Mboma, Dar es Salaam.
ZIKIWA zimebaki siku nne kabla ya kipenga cha Ligi Kuu Bara kuanza kutimua vumbi, uongozi wa Mbeya City umefunguka kuwa unahitaji kuanza kupata pointi tatu kuanzia mchezo wa kwanza mpaka msimu unapomalizika.


Utakuwa msimu wa tatu kwa timu hiyo ambayo safari hii itaanzia tena nyumbani kama misimu miwili iliyopita licha ya kushindwa kuondoka na ushindi na kuambulia sare mara mbili.
Msimu wa kwanza wa mwaka 2013/14 walifungua dhidi ya Kagera Sugar na walitoka sare 0-0, msimu uliofuata dhidi ya JKT Ruvu 0-0 kwenye uwanja huohuo na safari hii wanafungua kwa mara nyingine na Kagera Sugar.


Akizungumza na Championi Jumatatu, katibu wa timu hiyo, Emmanuel Kimbe, alifunguka kuwa, wanaanza nyumbani lakini wao wamejipanga kwa ajili ya msimu mzima na wamepania kuanza kuondoka na pointi tatu katika mchezo wa kwanza.

Kimbe alisema kuwa kikosi chao msimu huu kimefanya usajili wa uhakika, ingawa timu hiyo itakuwa na mabadiliko.
“Malengo yetu ni kufanya vyema zaidi msimu huu, ingawa ni wazi ushindani utakuwa mkubwa lakini upande wetu tunahitaji Mbeya City ianze kuchukua pointi tatu kuanzia mchezo wa kwanza mpaka wa mwisho bila kujali inacheza na nani.


“Misimu miwili mechi za ufunguzi hatujaondoka na pointi tatu na kucheza na Kagera kwa mara ya pili kwenye ufunguzi si tatizo, sisi zaidi tunaangalia jinsi ya kupambana na kuweza kufikia malengo,” alisema Kimbe.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.