Mwigulu Nchemba na Mwakalebela wakiwa
kwenye Gari ya wazi wakielekea Uwanja wa Mwembetogwa hapa Iringa Mjini
tayari kwa uzinduzi wa kampeni za Ubunge.
Mwigulu Nchemba akiingia na Gari la
wazi kwenye Viwanja vya Mwembetogwa hapa Iringa Mjini kwaajili ya
Kumnadi Mwakalebela anayepeperusha Bendera ya Chama Cha Mapinduzi kwenye
nafasi ya Ubunge.
Mwigulu Nchemba ambaye yumo kwenye
kikosi cha Timu ya Ushindi ya CCM,hapa akiwasili Viwanja vya Mwembetogwa
kwa ajili ya kuzindua Rasmi kampeni za Ubunge Jimbo la Iringa Mjini kwa
upande wa CCM

Sehemu ya Maelfu ya Wananchi wa Iringa
Mjini wakifuatilia Mkutano wa Uzinduzi wa kampeni za CCM Ubunge Jimbo
la Iringa Mjini hii leo.
Ombi la Mdahalo kati ya Wagombea Urais halikupitwa kwenye mkutano huu wa kihistoria kwa Wananchi wa Iringa.

Mwigulu Nchemba akizungumza na Maelfu
ya Wananchi wa Iringa hii jana katika Viwanja vya Mwembetogwa wakati
akifungua Kampeni za Ubunge Jimbo la Iringa Mjini ambapo CCM
imemsimamisha Mwakalebela.
Wananchi wakiwatayari kusikiliza sera za chama cha Mapinduzi kwa Jimbo la Iringa kuelekea miaka 5 ijayoya Ubunge.
Mwigulu Nchemba akiwasisitiza Wananchi
wa Iringa kuwa ,Taifa letu linahitaji Kiongozi Magufuli kwasababu
anasifa ya Uchapakazi, Mwadilifu, Mtanzania halisi,Sio mbaguzi na hana
Urafiki kwenye kazi.Hivyo watanzania wampigie Kura magufuli ifikapo
October 25 Mwaka huu.

Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Iringa Ndg.Mwakalebela
Mwigulu Nchemba akimuombea Kura mbunge Mtarajiwa wa Iringa Mjini Mh.Mwakalebela.
Ndg.Mahiga
ambaye ni meneja kampeni wa Mwakalebela akiwatoa hofu wananchi wa
Iringa kuwa watafanya Kampeni za Amani na Utulivu na amewahakikishia
wataibuka washindi mapema October 25.2015.
Mwakalebela
ambaye ni Mgombea Ubunge akizugumza na Wananchi wa Iringa Mjini.Kubwa
amesisitiza kuwa anazijua kero za Wananchi wa Iringa Mjini hususani
maji,Miundombinu na huduma za Afya,Hivyo yupotayari kuwatumikia kwa
miaka 5 ijayo kama Mbunge wao.
Mwigulu Nchemba akionesha alama ya “CCM ni Nambari 1”

Wananchi wa Iringa wakishangilia mara baada ya Mwigulu Nchemba kumsimamisha Mbunge Mtarajiwa Ndg.Mwakalebela.
Mwigulu Nchemba akiwambia Wananchi wa Iringa kuwa mambo yapo POA kuelekea uchaguzi Mkuu 2015.
Hisia za Wananchi kwa chama chao,Chama cha Mapinduzi.
Mwigulu Nchemba (katikati), Mbunge
mtarajiwa Mwakalebela (kushoto) na Kampeni Meneja wa Mwakalebela
Ndg.Mahiga(Kulia) wakiwaaga wananchi wa Iringa mjini na kuwashukuru kwa
Mafuriko waliyoyaleta Uwanja wa Mwembetogwa.
Picha na Sanga Festo Jr.

Note: Only a member of this blog may post a comment.