Saturday, June 13, 2015

Anonymous

Kocha SIMBA SC Hakijaeleweka!

Martha Mboma na Omary Mdose
HADI jana Ijumaa jioni, Simba ilikuwa ikiendelea kujadiliana kuhusu kocha wake mpya huku raia mmoja wa Uingereza akipewa nafasi kubwa ya kupewa kazi hiyo.

Rais wa Simba, Evans Aveva, alilithibitishia Championi Jumamosi kwa kusema: “Kocha mpya wa Simba ni raia wa Uingereza, mambo hayajakaa sawa tutawatajieni jina lake.”

Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa, klabu hiyo inafanya siri kumtaja kocha huyo hadi itakapofikia makubaliano naye kuepuka kumkosa kama ilivyokuwa kwa Kim Poulsen. Poulsen akiwa katika mazungumzo na Simba aliipa sharti la kutotajwa katika vyombo vya habari na pindi alipotajwa alikataa kuendelea na mazungumzo nao akidai hata akijiunga na timu hiyo siri nyingi zitavuja.Simba inataka kuleta kocha mpya kuchukua nafasi ya Goran Kopunovic raia wa Serbia aliyemaliza mkataba na kushindwa kuingia mkataba mpya.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.