Wilbert Molandi,Dar es Salaam
SIMBA imepiga hesabu za kuweka kambi yake Afrika Kusini katika kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, hata hivyo imesitisha uamuzi huo baada ya kuambiwa nchini humo kuna baridi kali ambayo haitawasaidia kufanya vizuri.
Matajiri wa Simba walikuwa wameshapiga hesabu za kwenda Afrika Kusini kuandaa kikosi chao ili kitishe msimu ujao lakini walipoambiwa baridi ya huko haifai, wameachana na mpango huo na sasa wanafikiri kwenda kwingine.
Kiwango cha hali ya hewa ya Afrika Kusini kwa sasa katika miji mingi ni nyuzi joto kati ya 6 hadi 22, wakati Dar es Salaam, Tanzania ni 25 mpaka 30.
Akizungumza na Championi Jumamosi, mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa wa uamuzi juu ya jambo lolote ndani ya Simba, alisema baridi kali ya Sauz imetibua kila kitu walichopanga. “Isingekuwa na maana yoyote kwenda kuweka kambi kwenye baridi halafu unakuja kucheza ligi kwenye joto, tulipanga twende Afrika Kusini kwa kambi ya wiki kadhaa lakini sasa mpango huo umekufa.“Kamati ya Utendaji imeketi na kupitisha uamuzi huo na sasa tunatazama mahali kwingine pa kuweka kambi huku tukiendelea na usajili,” alisema bosi huyo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.