Diddy amekamatwa na polisi kwa kudaiwa kupigana na kocha football wa chuo kikuu cha California, UCLA.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, polisi wa chuo hicho walimkata rapper huyo tajiri jana.
Mtoto wa Diddy, Justin Combs anachezea kwenye timu ya UCLA. Kocha
msaidizi alikuwa akimkalipia Justin uwanjani na Diddy hakupenda kiasi
cha kumfuata na kutaka kumdunda.
Anaendelea kushikiliwa kwenye kituo cha polisi cha chuo hicho.
Note: Only a member of this blog may post a comment.