Ni kama wametepeta vile ama watoto wa uswazi hupendelea kusema wamechora chini na imekula kwao hapa nawazungumzia ‘haters’, wazandiki na wanafiki a.k.a vizabinazabina wanaokesha wakiomba ‘couple’ maarufu yenye nguvu ya aina yake ya Kim Kardashian na Kanye West ivunjike.
Baada ya kusambaa uvumi kwa takriban mwezi mmoja sasa kwamba wanandoa hawa wapo mbioni kuachana baada ya kuzuka kwa madai kwamba Kim yupo kwenye mchakato wa kudai talaka na kuiomba mahakama impe mamlaka kamili ya kulea watoto wake (North na Saint) ni wazi sasa uvumi huo umesambaratishwa kwa tukio la hivi karibuni baada ya wawili hao kuonekana wakiwa pamoja.
Tangu Kanye alazwe hospitali na baadaye kuruhusiwa, kwa mara ya kwanza wametoka ‘out’ pamoja na Kim kwenda katika moja ya mgahawa huko Santa Monica kupata chakula cha usiku huku mwanamitindo huyo akiwa kavalia vizuri bila kusahau pete yake ya ndoa jambo lililozima fununu za kuachana kwao.

Note: Only a member of this blog may post a comment.