Je, ni kweli anatoka familia namba moja Tanzania au ni majina tu na fitina za wabongo?!
Tupe maoni yako hapo chini tafadhali!
Chanzo: JF
UCHAMBUZI KUMUHUSU JESCA JOHN MAGUFULI
KWANINI SERIKALI ILIPOTIMUA WALE "VILAZA" (FORM FOUR FAILURES) WALIOKUA WAMEJAZANA VYUO MBALIMNALI KIKIWEMO ST.JOSEPH, MBONA HAWAKUSHUGHULIKA NA JESCA? JE YEYE ANA "IMMUNITY?".
MASWALI "FIKIRISHI" vs MASWALI "CHOKONOZI.!"
Na Malisa GJ,
Rafiki yangu Comrade Rashid Chilumba kaniuliza maswali yaliyonitoa jasho kidogo. Maswali ya kufikirisha.
Katika kuchangia hoja ya binti anayedhaniwa kuwa ni mtoto wa Rais Magufuli aitwae "Jesca John Magufuli" Comrade Chilumba ameniuliza maswali kadhaa na kunitaka niweke ushahidi (Evidence) wakati nikijibu maswal hayo.
Sehemu ya maswal hayo Chilumba anauliza, Je huyo binti anayetajwa kwa jina la Jesca Magufuli ni mtoto wa Rais Magufuli kweli au ni mfanano wa majina? Kuna ushahidi wowote kuwa Magufuli ana mtoto aitwae Jesca? Kama yupo, je ana uhusiano na Jesca anayetajwa kusoma St.Mathew's?
Anahoji Chilumba na kuendelea; Je Jesca aliyedahiliwa UDOM na yule wa St.Mathew's ni mtu mmoja? Je hayo matokeo yanayodaiwa kuwa ni ya Jesca sio editing? Kwanini picha ya matokeo inayotembea mtandaoni ni moja tu?
Nimeyapenda maswali haya ya Chilumba kwa sababu yamenifanya "nifikirie sana" na mimi napenda kufikiria (Thinking is my hobby).
Maswali ya Chilumba yana mantiki sana kwa sababu jibu lolote kati ya maswali hayo linaweza kubadilisha mijadala yote inayoendelea mitandaoni kuhusu Jesca.
Kwa mfano swali la kwanza la Chilumba majibu yake yakiwa ni HAPANA basi yote tunayojadili huku mtandaoni ni bure. Yani kama Magufuli hana mtoto aitwae Jesca basi tunapoteza muda kujadili mambo ambayo ni "dhahania"
Na ikiwa jibu la kwanza litakua HAPANA basi hata hayo maswali mengine yaliyobaki yanakuwa hayana maana (yanakufa naturally). Huo ndio utamu wa critical thinking.
Kwa hiyo nimpongeze Comrade Chilumba kwa maswali haya mazuri ambayo yamedhihirisha kwamba alikua hasinzii kwenye vipindi vya Critical Thinking vya mwalimu wake Crispin Isaboke.
#MAJIBU
Nimefanya utafiti kidogo na kupata majibu ya maswali ya ndugu Chilumba. Nami napenda kuyajibu kama ifuatavyo kwa kuambatanisha na evidence kama alivyohitaji;
1. #SwaliLaKwanza
Je Rais Magufuli ana mtoto aitwae Jesca John Magufuli?
#JIBU
Ndio. Jesca John Magufuli ni mtoto wa kuzaliwa wa Mhe.Rais John Magufuli na mkewe Janeth Magufuli. Rais Magufuli ana watoto 7. Watatu wa kiume na wanne wa kike.
#Evidence
Katika orodha ya kuzaliwa Jesca ni mtoto wa 4. Watoto wengine wa Rais Magufuli ni kama ifuatavyo;
1. Suzzan John Magufuli
2. Edna John Magufuli
3. Joseph John Magufuli
4. Jesca John Magufuli
5. Lucy John Magufuli
6. Jurgen John Magufuli
7. Jerry John Magufuli
#EvidenceNunber2
Tembelea anuani hii ya Ikulu kufahamu zaidi juu ya familia ya Rais Magufuli na familia yake, http://www.ikulu.go.tz/index.php/state_house/about_president
2. #SwaliLaPili
Je Jesca ambaye ni mtoto wa Rais Magufuli amesoma sekondari ya St.Mathew kwa kipindi tajwa?
#JIBU
Ndio. Jesca John Magufuli binti wa Mheshimiwa Rais Magufuli amesoma sekondari ya St.Mathew na kuhitimu kidato cha 4 mwaka 2011.
#Evidence,
Mkurugenzi wa shule hiyo Bw.Thadeo Mutembei anaweza kudhibitisha hilo. Unaweza kumpigia kupitia simu yake nambari 0754 698845.
3. #SwaliLaTatu
Je, Jesca Magufuli aliyepata division four ya alama 30 ndiye huyo mtoto wa Rais Magufuli? (Au ni mwingine).
#JIBU
Ndiye huyo.
#Evidence;
Hakukuwa na Jesca Magufuli wawili katika sekondari ya St.Mathew.
4. #SwaliLaNne
Je matokeo yanayosambazwa mitandaoni kwamba ni ya Jesca ni matokeo halisi au ni photoshop?
#JIBU
Ni matokeo halisi, hakuna photoshop wala editing.
#Evidence
ingia kwenye website hii utaona matokeo yote ya sekondari ya St.Mathew's kwa mwaka 2012 na utaona jina la Jesca katika orodha hiyo. Nambari yake ya mtihani ilikua S.1071/102 http://196.44.162.33/necta2011/CSEE%202011/s1071.htm
#SwaliLaTano
Je ni kweli kuna mtu aitwae Jesca Magufuli alidahiliwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mwaka 2014 kusomea shahada (degree) ya biashara ktk Rasilimali watu?? (Bachelor of Commerce in Hunan Resource Management).??
#JIBU
Ndio. Mwaka 2014 miongoni mwa wanafunzi waliodahiliwa kujiunga na Cho Kikuu cha Dodoma ni binti mmoja aliyejulikana kwa jina la Jesca John Magufuli.
#Evidence
Ingia kwenye website hii kisha tafuta Admisdion number 230. Pitia hapa http://41.93.31.136:8080/Selections/UnderGraduate.jsp…
6. #SwaliLaSita
Je, Jesca Magufuli aliyedahiliwa UDOM mwaka 2014 ndio yule Jesca aliyemaliza St.Mathew's mwaka 2011 ambaye ni mtoto wa Rais Magufuli.
#JIBU
Ndiyo. Jesca anayesoma UDOM ndiye Jesca yuleyule aliyemaliza kidato cha 4 mwaka 2011 sekondari ya St.Mathew ambaye pia ni mtoto wa Rais Magufuli.
#Evidence
Unaweza kumpigia Mkuu wa Chuo cha UDOM Prof.Idrisa Kikula kudhibitisha kama kweli Jesca Magufuli aliyepo chuoni hapo ndiye yule binti wa Mheshimiwa Rais Magufuli. Namba ya Prof.Kikula ni 078 455 5655.
#HITIMISHO
Comrade Chilumba nafikiri nimekujibu maswali yako yote kama ulivyoniuliza. Na nimejitahidi kukupa evidence kama ulivyonitaka kufanya hivyo.
Sasa nakuomba na wewe unisaidie vimaswali vyangu vidogo kama ifuatavyo;
1. Hivi ilikuaje Jesca akasoma degree wakati alipata Division four ya point 30?
2. Je ana foundation course yoyote labda Diploma? Kama anayo amesomea chuo gani? Na aliwezaje kupata diloma ndani ya miaka miwili? Ina maana hakusoma certificate?
3. Na ilikuaje Udahili wake wa UDOM ukapitia NACTE wakati muongozo wa NACTE wa mwaka 2005 unazuia vyuo vilivyopo chini yake kudahili wanafunzi wenye alama chini ya 28?? Yeye ana 30 alidahiliwaje?
4. Amewezaje kusoma Bachelor of Commerce wakati somo la Commerce alipata "F" kidato cha 4??
5. Kwanini Serikali ilipotimua wale "Vilaza" (Form four failures) waliokua wamejazana vyuo mbalimnali kikiwemo St.Joseph, mbona hawakushughulika na Jesca? Je yeye ana "immunity??"
6. Je kauli ya Mheshimiwa Rais wetu mpendwa JPM kwamba kuna watoto wa vigogo waliofeli form four wamejazana vyuo vikuu na kuziba nafasi kwa watoto wa maskini wenye sifa na vigezo, je haimlengi Jesca? Hasa ukizingatia kuwa yeye ndiye mtoto wa kigogo mkubwa zaidi nchini? (Mtoto wa Mheshimiwa zaidi). Kama haimlengi Jesca ilikua inalenga akina nani?
Tafadhali Comrade nisaidie majibu ya viswali vyangu hivyo hapo juu. Naamini viswali vyangu hivi sio vigumu kama maswali yako ya Critical Thinking.
Chanzo : Malisa Godlisten E.J
Note: Only a member of this blog may post a comment.