Tuesday, June 23, 2015

Anonymous

BABA LEVO Adai Hajafulia Kimuziki!

Baba Levo amesema hajafulia kimuziki kama watu wanavyodhani.

Akizungumza na Bongo5, Baba Levo amesema kama angekuwa amefulia kimuziki angeshindwa kulipia nyumba anayoishi ambayo amedai analipa milioni 9 kwa mwaka.

“Mimi sijafulia, mtu akifulia hata media zinamuogopa hana cha kusema,” amesema.

“Mimi ni mjasiriamali, muziki umebadilika na mimi nika change wala sijapoteza mwelekeo. Nina miaka 14 kwenye huu muziki, mimi sijakiki kama shetani na siwezi kushuka nikawa kama mwendawazimu kwahiyo mimi nipo katikati. Kwenye biashara kuna vitu viwili unaweza ukapata pesa ya kuweza kujikimu mwenyewe kimaisha au unaweza kutapata pesa nyingi ukaanza kufanya kufuru kama wengine. Mimi kipato changu kinaendesha maisha yangu ya kawaida, maisha hayaendeshwi na kula tu, kuna vitu vingi ambavyo vinaendeshwa kwenye maisha, mimi nakaa nyumba karibia laki 700,000 kwa mwezi, kwa mwaka ni karibu milioni 9,000,000, hii ina maana muziki wangu unawezesha kuendesha maisha yangu familia yangu pamoja na watoto wangu. Levo namlipia ada ya milioni 3,500,000 kwa mwaka, so ukipiga hesebu yangu kwa mwaka ni mamilioni ya hela, kwahiyo kama ni mtu wa kawaida kawaida huwezi kulipa,” amesisitiza rapper huyo.

Pia Baba Levo alisema amejipanga kuachia wimbo wake mpya uitwao Bwege ambao unazungumzia vijana wanaoshindwa kuthamini ndugu zao na kuthamini wasichana.

“Naachia wimbo wangu mpya unaitwa Bwege na sasa hivi nipo kwenye harakati za kufanya video kali sana, wimbo unazungumzia mazingira ya mtu anapokuwa anamhudumia mpenzi wake. Kuna baadhi ya watu wanaona huyu ni mjinga sana, unawezaje kumnunulia mpenzi wako saa ya dhahabu wakati mama yako na dada yako hujawahi kumfanyia kitu kama hicho. Kwahiyo unaonekana kama ni bwege.”
-via bongo5

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.