Monday, January 2, 2017

Unknown

Sio Chid Benz Tu Tazama Hali ya Nando (Mshiriki wa BBA) Baada ya Kuathirika na Matumizi ya Madawa ya Kulevya!

Huyu ndio kijana mwingine anayetoa "alarm" kwa vijana wa kisasa kuwa dawa za kulevya sio "ujanja" ni majanga. Unaweza kuanza na kuvuta kisirisiri, lkn majibu ya madhara yake yakawa hadharani na unapotoka hadharani basi muda unakuwa umekwisha kwenda.
Tuwasaidie vijana wetu waepukane na matumizi ya madawa ya kulevya.
 

Staa huyu aliyewahi kuiwakalisha Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa – The Chase, Nando ameendelea kudhoofika kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. 
Muonekano wa zamani wa Nando
Nando aliyewahi kudai kuachana na matumizi ya dawa za kulevya, alikuwa kipenzi cha wasichana wakati anashiriki kwenye shindano hilo na alitazamiwa kushinda kabla ya kutimuliwa kutokana na kujihusisha kwenye ugomvi kwa kumtishia kumchoma kisu mshiriki wa Ghana.
Mwishoni mwa wiki, picha inayoonesha muonekano wake wa sasa imesambaa mtandaoni na kuwashtua watu wengi.
Muonekano wa sasa wa Nando
Mwaka uliopita staa mwingine aliyeikilisha Tanzania katika shindano hilo, Feza Kessy, alisema kuwa anaamini Nando amepatwa na tatizo au anaugua kwakuwa tabia anazozionyesha zinampa mashaka.

Akiongea kwenye kipindi cha Kubamba kupitia Times FM, Feza alisema anaona akili ya Nando kama imevurugika kwa sasa. Alisema amekuwa tofauti na Nando, yule kijana mwenye nidhamu na mpole aliyekuwa akimfahamu.
“Naamini Nando ana tatizo asaidiwe,” alisema Feza. “Sijui kwanini lakini naamini Nando ana something hayupo sawa, sio yule Nando ninayemfahamu, naomba atafutwe asaidiwe,” alisisitiza.  
Feza Kessy na Nando
Feza ambaye kwa sasa ni mtangazaji wa Choice FM, alidai kuwa aliwahi kukutana na Nando na akampa noti ya shilingi elfu 10. Anasema badala yake yake staa huyo aliitupa chini kwa madai kuwa haiwezi kumsaidia kitu.

Kabla ya hapo Nando aliwahi kudai kuwa atatoa kitabu chake kiitwacho ‘Mhuni huyo Mwenye Akili.  
“Sababu ya kuingia huko, ni ujana tu mwanangu…unajua ujana ni maji ya moto kama watu wanavyosema. Na pee pressure na watu niokuwa nao wakati ule, na life nililoishi mimi…ni yale maisha ya kujiachia,” Nando alikiambia kipindi cha Hatua Tatu cha Times FM kuhusu kilichomfanya ajiingize kwenye matumizi ya dawa hizo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.