Thursday, December 22, 2016

Unknown

Nchi Zote Justin Bieber Atakwenda Lakini Hii Hakanygi Ng'o!

Superstar mzaliwa wa Canada mwenye umri wa miaka 22 pekee, Justin Bieber anaweza kusafiri nchi zote duniani kwa utalii na kupitia kazi zake za muziki lakini ipo nchi moja tu ambayo liwe jua iwe mvua, uje mchana ama usiku, si kiangazi wala masika Bieber ataweza kukanyaga ardhi ya nchi hiyo.

Nchi hiyo si nyingine bali ni Argentina huko anapotokea Lionel Messi msakata kabumbu anayekipiga kunako Klabu ya Barcelona kwa sasa. Bieber hawezi kukanyaga nchi hiyo kutokana na kuhofia kutiwa nguvuni baada ya kumwagiza mmoja wa walinzi wake kumwangushia kichapo mmoja wa wapiga picha nchini humo.

Kwa mujibu wa Mtandao wa TMZ Justin Bieber hafikirii kukanyaga Argentina kwa sasa hadi pale kesi yake itakapopata ufumbuzi ingawa kwa sasa kikwazo anachokumbana nacho ni ‘tour’ yake ya Kusini mwa Amerika anayotarajia kuifanya hivi karibuni ambapo Argentina ni moja ya sehemu ambayo itamwingizia mtonyo mrefu kutokana na kuwa na ‘funbase’ kubwa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.