HATARI SANA: WAWEKEZAJI WA KICHINA WANAVYOCHOMA MISHIKAKI TANZANIA!
UWEKEZAJI
wa Wachina nchini Tanzania umelalamikiwa na wananchi kwa watu hao
kufanya biashara za rejareja kama vile kuchoma mishikaki, kuuza nguo,
simu na vitu vingine mitaani, jambo ambalo linawanyima fursa wenyeji
wasio na uwezo wa biashara kubwa.
Katika
maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam si ajabu kukutana na baadhi
ya Wachina wakiwa na biashara mikononi kama wafanyabishara wadogo nchini
humo maarufu kama Machinga, hali inayozua mshangao na viulizo kwamba
kweli hawa ni wawekezaji ama wamegeuka kuwa wafanyabiashara ndogo ndogo!
Eneo la kibiashara la Kariakoo jijini Dar es Salaam ni mfano hai wa
jinsi watu wa mataifa ya nje, zaidi ya Wachina, ambao wanafanya biashara
za kawaida kama vile maduka madogo ya kawaida ambayo yanamilikiwa na
Watanzania wa kawaida wenye mitaji midogo.
Swali ambalo Watanzania wanajiuliza ni kwamba wageni hawa ‘Machinga’
ni wawekezaji au ni watu waliokwepa macho ya serikali na kuingia mitaani
kuwazibia riziki Watanzania! Kama wanafanya hivyo kinyemela, ni nani
hasa mwenye mamlaka ya kuweza kuwaondoa mitaani na kuhakikisha
‘uwekezaji’ wa aina hii unaondoka mitaani?
CHANZO: BBC SWAHILI
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Note: Only a member of this blog may post a comment.