Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuwa adui yake namba moja ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha Alliance for Change and Transparance (ACT-wazalendo), Zitto Kabwe.
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, John Mnyika
akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Furahisha Mwanza
juzi, alisema Chadema haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo ndani ya
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutokana na kile alichosema ‘ni adui kwao’.
“Mtume
Muhamad (S.A.W) alikuwa anazungumzia unafiki ambao una sura mbili na
sifa zake, leo (ACT) wanasema wapo upinzani, wanasema msiunge mkono
Ukawa halafu mnawakaribisha?
“Nendeni
kila mahali waambieni wananchi adui yetu mkuu ni Zitto. Sikilizeni
niwaambie Taifa hili kama ni ufisadi tumeshazungumzia sana kuanzia EPA
mpaka Richmond. Dk. Slaa (Willbrod) alipoingia bungeni aliyasema haya
kwa sasa si mapya. Adui yetu ni Zitto na hatumtaki Ukawa,”Mnyika.
Zitto alisema pamoja na hali hiyo,
ACT-Wazalendo haiko tayari kuzungumzia siasa za wakati uliopita kwa vile
kufanya hivyo si afya njema kwa siasa za upinzani.
“Mwanzo walipotufukuza walituambia tukatafute vyama vingine hilo
likafanyika, tulipopata vyama vya kufanyia siasa wakasema vipo kwa ajili
ya kugawa upinzani tukasema tupo tayari kuunganisha nguvu ya pamoja kwa
ajili ya kuiondoa CCM…wenzetu pia hili hawalitaki sasa ni wajibu wenu
kutambua watu gani hawataki kuiondoa CCM,” Zitto.
Zitto ambaye amefuatana na Mwenyekiti wa
chama hicho, Anna Mghwira, waliwasili Mwanza saa 8.00 mchana na kupata
mapokezi makubwa yaliyoanzia wilayani Misungwi.


Note: Only a member of this blog may post a comment.