Thursday, April 14, 2016

Anonymous

DAYNA Nyange Amuonea Wivu ROMA Mkatoliki!

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwanaisha Nyange ‘Dayna Nyange’.
Stori: Boniphace Ngumije
MWANADADA anayefanya poa kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Mwanaisha Nyange ‘Dayna Nyange’ hivi karibuni amedai kuwa anamuona wivu staa wa Hip Hop, Roma Mkatoriki kutokana na hatua aliyoifikia ya kufunga ndoa Jumamosi iliyopita mkoani Tanga na mchumba wake wa muda mrefu.

Dayna anasema amekuwa mtu wa karibu wa Roma kwa muda mrefu sasa ambapo amewafahamu wapendanao hao tangu mwaka 2008 na anashukuru kuona wametimiza ahadi yao ya kuoana lakini kwake pia hiyo ni changamoto ya kuhakikisha pia anaingia kwenye ndoa.
“Roma amefanya kitu cha msingi, ninamuonea wivu kuingia kwenye maisha ya ndoa na ninafikiri amenikumbusha pia kutakiwa kulitimiza hilo jukumu,” alisema Dayna Nyange.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.