Sunday, November 22, 2015

Anonymous

Ya MUNGU Mengi: Msaada Wahitajika Kwa Mapacha Hawa Walioungana Wilayani Ngara

Mapacha wakiwa wameungana.
Hawa watoto Zahra na Zarina wamezaliwa pacha walioungana tarehe 16/11/15 mama yao Bi Tausi Hageze akiwa njiani kwenye boda boda akitokea kijiji cha Nyarurema Tarafa ya Rulenge Wilaya ya Ngara akielekea hopitali ya misheni Rulenge. Alipopata uchungu wa kuzidi alimuomba bodaboda asimame akaweza kujifungua kwa shida mbele ya mumewe anaeitwa Hamdani hapo njiani.

Baada ya hapo wakapelekwa hospitali ya misheni Rulenge. Mama na watoto wako salama, kama unavyoona katika picha wameungana kiunoni. Msamaria amekutana na changamoto hii hapo hospitali na kuamua kuwasaidia kuchangisha ili wapelekwe Mwanza Bugando Hospital walipo hivi sasa.

Inaelezwa na madaktari hapo wameshauri watoto wapelekwe India kwa upasuji na matibabu zaidi.

Msamaria anaewasaidia Bi Sabra Said Salum wa namba ya simu +255767220099 anaomba yoyote atakaeguswa na kadhia hii afikishe mchango kwake ili aweze kuwafanyia safari hii muhimu kuokoa maisha ya mapacha hawa.

Baba Hamdani Sibhoro na mama Tausi Hageze wote ni wakulima wa jembe la mkono hawana uwezo hata wa kufika Dar. Bi Sabra kachangisha na kuweza kuwafikisha Bugando, kuwalipia mahitaji ya hapo.
Mungu awabariki

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.