Sunday, November 22, 2015

Anonymous

Maporomoko ya Udongo Yaua Watu 90, Wengine Kadhaa Hawajulikani Waliko!

IDADI ya watu waliofariki kutokana na maporomoko ya udongo katika eneo la Jade nchini Myanmar imeongezeka na kufikia watu 90, huku wengine kadhaa wakiwa hawajulikani waliko. Ofisa mmoja katika jimbo la kaskazini la Kachin anasema kuwa waokoaji wanaendelea kuopoa miili zaidi. 

Watu wengi waliopoteza maisha walifunikwa wakati mlima wa taka zilizorundikwa na makampuni ya kuchimba migodi ulipoporomoka.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema waliopoteza maisha wengi wao ni wazoaji taka wanaoishi karibu na eneo hilo ambao hutafuta vifaa kwenye taka kwenda kuuza.
Credit: BBC

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.