Friday, November 20, 2015

Anonymous

Rais MAGUFULI Amuapisha Kassim MAJALIWA Kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, muda huu amemuapisha Mbunge wa Ruangwa, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania mjini Dodoma

Hafla ya Kumuapisha Mh. Majaliwa imefanyika kwenye Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo, Makamu wa Rais wa Tanzania, Bi. samia Hassan Suluhu, Rais wa Zanziba, Dk. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Rais Msitaafu, Dk. Gharib Bilal, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, Wabunge, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, Wabunge na wageni wengine.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.