Naibu
Spika, Dk. Tulia Ackson, amekalia kiti hicho kwa kuanza kuonja 'joto la
jiwe' baada ya kushindwa kujibu swali lililomtaka aeleze muda gani
aliojiunga na Chama cha Mapinzuduzi (CCM) huku akikumbana na zomea zomea
kali kutoka kwa wabunge wa vyama vya upinzani.
Mtafatuku
huo uliibuka ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana, wakati Dk.
Tulia alipokuwa akijinadi kwa wabunge kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi wa
Naibu Spika.
Nafasi
hiyo ilikuwa ikiwaniwa pia na Mbunge wa Kaliua (Cuf), Magdalena Sakaya,
ambaye kura 101 alizopigiwa hazikutosha kumfanya akalie kiti hicho
dhidi ya Dk. Tulia aliyepata kura 250.
Hata
hivyo, swali lilosababisha bunge hilo kuvurugika lilitoka kwa Mbunge wa
Tarime Mjini, Esther Matiko (Chadema), ambaye alimtaka Dk. Tulia atoe
ufafanuzi muda wa uanachama wake ndani ya chama hicho, na kama mtumishi
wa serikali ataje siku aliyotangaza kuachia ngazi na kujiunga na CCM
kwani sheria na kanuni za utumishi wa serikali inamzuia kujiunga na
chama chochote cha siasa.
“Nakuomba
utulieleze sisi wabunge kwa kuwa wewe ulikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa
Serikali na kwa mujibu wa sheria inafahamika wazi kuwa mtumishi wa
serikali hasa katika ngazi yako hukutakiwa kuwa mwanachama wa chama cha
siasa. Tunaomba utuambie lini ulijiunga na CCM, hasa kwa ukizingatia
hivi karibuni ulisimamia kesi ya mita 100,” aliuliza Matiko.
Swali
hilo lilimfanya Spika Job Ndugaye ambaye alikuwa akiendesha kikao hicho
kuwauliza wabunge kama linafaa kujibiwa. Wabunge hasa wa upinzani
walijibu kwa sauti kwamba hilo ni swali na linapaswa kujibiwa.
“Mheshimiwa Dk. Tulia haya jibu swali hilo,” Ndugai alimtaka kujibu.
Dk.
Tulia wakati akijibu alionekana kutumia muda mwingi kufafanua vifungu
vya katiba na sheria vinavyozungumzia zuio hilo, jambo ambalo wabunge wa
kambi ya upinzani walionekana kutoridhika nalo.
“Kama
ulivyosema mimi ni mwanasheria, katiba nimeisoma, sheria
zinazozungumzia utumishi wa umma nimezisoma na kanuni zake
nimezisoma…nasema hivi kanuni nimezisoma, sheria nimezisoma,” alisema na kukatishwa na sauti za wabunge zikimtaka kujibu swali.
Kutokana
na hali hiyo, Spika Ndugai aliingilia kati kwa kuwaomba wabunge kuacha
kumzonga mgombea na vizuri wangemsikiliza kama walivyofanya wakati
Sakaya akijinadi.
“Mheshimiwa
spika yapo makundi matatu ya watumimishi wanaokatazwa kuwa wanachama na
vyama vya siasa, kwanza ni wanajeshi ambao ni polisi na wanao…,” alijibu Dk. Tulia na kukatishwa na zomeazomea kutoka kwa wabunge.
Hata hivyo, Spika Ndugai alisimama na kumuamuru Katibu wa Bunge kuendelea na taratibu za uchaguzi.
Baada
ya uchaguzi, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, alimtangaza Dk.
Tulia mshindi baada ya kupata kura 250 sawa na asilimia 71.2 wakati
Sakaya akipata kuta 101 ambazo ni sawa na asilimia 28.8 za kura zote.
Alisema wabunge wote waliosajiliwa walikuwa 369, lakini idadi ya waliopiga kura ni 351.
Kutokana
na matokeo hayo, Spika Ndugai alimtangaza Dk. Tulia kuwa Naibu Spika wa
Bunge hilo na kumuapisha rasmi kuanza kazi yake hiyo mpya.
Note: Only a member of this blog may post a comment.