Saturday, October 3, 2015

Anonymous

Hivi ni Kweli LOWASSA Analipa Kisasi?

Nimetafakari maneno aliyoandika mwandishi wa gazeti la Raia mwema ndugu Johnson Mbwambo, kwenye toleo la wiki hii Na.425. Anasema kitendo cha Lowassa kujiunga na Chadema, chama ambacho kwa miaka mingi kimekuwa kikimtuhumu kwa ufisadi ni kulipa kisasi. 
Kwa maana sasa hivi Lowassa amekuwa aki-enjoy kuona jinsi wakina Lissu na Mbowe wanavyohaha majukwaani kumsafisha baada ya wao wenyewe kumchafua, kwake huo ni ushindi mkubwa hata kama atashindwa uchaguzi.

Pia kwa upande mwingine ni kulipiza kisasi kwa CCM waliomkata, na sasa wanahaha kupambana na Chadema. Hata akishindwa atarudi kijijini kwake kama shujaa aliyewashikisha adabu adui zake...
Swali Langu :
Hivi ni kweli Lowassa analipa kisasi?

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.