SIKU
chache baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitisha kanuni ya
timu zote za Ligi Kuu Bara kuwakatia bima ya afya wachezaji wake, sasa
nyota hao watakuwa wakipatiwa matibabu ya akili bure.
Miongoni mwa wachezaji watakaopatiwa huduma hiyo ni straika wa Yanga, Donald Ngoma na beki kisiki wa Azam FC, Pascal Wawa, ambao shughuli huwa kubwa kila wanapokutana.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Rehani Athuman, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, tatizo la akili ni tatizo kubwa na linawasumbua wachezaji wengi duniani.
Kwa kuanzia, Athuman alisema wachezaji watakuwa wakipatiwa huduma hiyo ya matibabu kabla na baada ya michezo ya Ligi Kuu Bara.
“Mbali na huduma hiyo, pia kuna huduma nyingi za kiafya ambazo watakuwa wakipata pindi watakapokuwa na matatizo.
‘’Vilevile hata huduma ya lishe pia tutakuwa tunawapatia ambapo tutawapa ushauri wa aina gani ya chakula wanachopaswa kula kwa lengo la kujenga miili yao na hii itategemea utayari wao na viongozi wao,” alisema Athumani.
NHIF imeingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kutoa huduma ya bima ya afya kwa wachezaji na watu wa benchi la ufundi kwa timu 16 za ligi hiyo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.