MTOTO
mzuri Bongo Movies, Jacqueline Wolper, amejikuta akiambulia matusi
mazito kutoka kwa staa mwenzake Isabela Mpanda kisa kikiwa ni kuonesha
mapenzi yake kwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Edward Lowassa.
Isabela aliamua kumtusi staa huyo akidai
anamshanga kujinadi kila siku katika mtandao wa Instagram kuwa ni
mfuasi wa Lowassa wakati amelelewa na Chama cha Mapinduzi (CCM).
“Huyu naye paka gani (Wolper) anajitia
anaiponda CCM wakati njaa zake anaponea CCM. Panya Road wewe kwani
anafanya nini koko huyu mpuuzi mkubwa, ms…,” aliandika Isabela kwenye
Instagram.
Baada ya Isabela kumporomoshea matusi
hayo, mtu wa karibu na Wolper alidai suala hilo lilimnyima raha kiasi
cha kujuta kuonesha mapenzi yake kwa Lowassa.
“Wolper amejuta. Amesikitishwa na matusi hayo ambayo ameyaona hayakumstahili,” alisema mtu huyo wa karibu na Wolper.
Alipotafutwa Wolper kuhusiana na ishu hiyo, alikiri kuona matusi hayo na kudai alimpuuza maana si mtu wa hadhi yake.
“Mpuuzi huyo. Nimempuuza maana hata simu
yake anayotumia kuandikia huo ujinga na yangu hazifanani. Simu yangu
haina hadhi ya kumjibu mtu mwenye simu za kimaskini,” alisema Wolper.

Note: Only a member of this blog may post a comment.