Saturday, September 12, 2015

Anonymous

Hans POPPE Ahoji Mamilioni ya YANGA SC

POPE1
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, ameibuka na kuamsha jambo jipya sana, kwamba wapi ambako watani wao Yanga wanatoa mamilioni ya fedha na kufanya usajili.
Hans Poppe amesema Yanga imekuwa klabu inayopandisha kwa kasi kubwa fedha za mishahara na zile za usajili wa wachezaji kutoka nje, jambo linalofanya ajiulize, wanatoa wapi hizo fedha?

Katika mahojiano maalum na Championi Jumamosi, Hans Poppe amesema Simba na Yanga ni klabu ambazo vyanzo vyao vya mapato vinalingana kabisa.
“Lakini wenzetu wamekuwa wakiwalipa wachezaji hasa wa nje zaidi ya mara mbili. Jambo ambalo linaonyesha wazi kuna kitu, najiuliza wanatoa wapi fedha?

“Tambwe ambaye amekuwa akilipwa dola 800 (Sh milioni 1.6), Yanga nasikia wanamlipa dola 2,000 (Sh milioni 4). Najiuliza sana, kwamba tunapokwenda ni tatizo pia,” alisema Hans Poppe.
“Angalia wachezaji wa Burundi tulikuwa tukiwasajili kwa fedha ya chini, Yanga wameingia na papara na kupandisha sana masuala ya usajili.

“Nakumbuka hata Azim Dewji na Abbas Guramali walipandisha sana fedha za mishahara na usajili. Baada ya wao kuondoka, waliobaki walisumbuka sana.
“Ningependa kuwaasa viongozi wa Yanga kuliangalia hilo au Yanga iwe makini kwamba kweli fedha hizo zinazotoka ni zile zinazotokana na kipato chao.

“Hauwezi ukawa mfanyabiashara makini halafu ukawa unalipa zaidi ya kile unachoingiza na hili ndilo swali langu la msingi,” alisisitiza Hans Poppe.
“Najua kwenye hizi klabu kuna watu wanasaidia, lakini najua si kwa namna hiyo.” 


Hans Poppe alisema msimu huu, usajili wa Simba umefanyika kwa kufuata utaratibu na bajeti ambayo inaingia ndani ya kipato cha Simba.

“Kweli, hatukutoka nje ya kipato chetu. Ni usajili ambao umefiti ndani ya kipato cha Simba,” alisisitiza Hans Poppe.
Simba inafungua dimba la Ligi Kuu Bara dhidi ya African Sports katika mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, leo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.