Saturday, September 12, 2015

Anonymous

MGOSI: Hii siyo SIMBA SC ya Sare, Tunaitafuna African Sports

musa-hassan-mgosi
NAHODHA wa Simba, Mussa Mgosi amekataa sare katika timu yake na kusema wamejiandaa kutoa dozi katika mechi za Ligi Kuu Bara kuanzia na hii ya leo dhidi ya African Sports ya Tanga.
Msimu uliopita wa ligi kuu, Simba ilianza kwa kutoa sare mfululizo kiasi cha kutishia ushiriki wake katika michuano hiyo kabla ya kuzinduka na kushika nafasi ya tatu.

Mgosi aliliambia Championi Jumamosi kuwa, kwa kuanzia wataanza kufanya vizuri leo kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga dhidi ya African Sports licha ya kuwepo na ugumu katika mchezo huo.
“Simba ya msimu huu siyo ile ya msimu uliopita kwani imezaliwa upya kutokana na mabadiliko makubwa yaliyofanywa na uongozi na kocha (Dlyan Kerr), mashabiki waje uwanjani waone mambo.

“Hii siyo ile Simba ilikuwa ikitoa sare nyingi bila mpango, msimu huu tumekuja kivingine. Tunajua mashabiki wanataka nini na ndicho tutakachokifanya na tunaanza na African Sports,” alisema Mgosi.
Licha ya cheo cha unahodha, Mgosi ni miongoni mwa mastraika wa Simba akiwa anasaidiana na Hamis Kiiza kutoka Uganda, Ibrahim Ajib na Pape Abdoulaye N’daw raia wa Senegal.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.