Kama imekupita Hekaheka ya leo MAY 02 2015
inahusu mwanamke mmoja ambaye amesema kwamba mume wake alikuwa anamdai
kila siku mtoto.. akaamua aingie Hospitali ya Mwananyamala kwenye wodi
ya Wajawazito, akajifanya na yeye ni mjamzito.
Baada ya kukaa kwa muda wanawake wenzake
walimshtukia alikuwa kwenye pilika pilika za kutaka kuiba mtoto,
walipopeleleza wakajua kwamba hakuwa mjamzito na alikuwa na mpango wa
kuiba mtoto.. ishu ikafika Polisi na kwa sasa bado kesi iko mikononi
mwao.
Geah Habib
anaifuatilia hii na tutasikia zaidi kuhusu ishu hiyo kwenye Hekaheka
zinazofuatia.. kilichosimuliwa leo kiko kwenye hii sauti hapa chini mdau....

Note: Only a member of this blog may post a comment.