Nuh Mziwanda amedai kuwa kabla Shilole hajaondoka kwenda nchini Marekani walimalizana kila kitu na BASATA.
Nuh amesema vibali alivyochukua Shilole BASATA ndio vilivyomwezesha kuchukua visa ya kusafiria.
“Ili upate urahisi wa kupata visa lazima upate vibali vyote vya
BASATA,” Nuh aliambia XXL ya Clouds FM. “Kwahiyo ilibidi awe na vibali
vyote vya BASATA kwasababu BASATA walizungumza na Msando yakaisha pale
pale,” aliongeza.
Hata hivyo Katibu Mtendaji wa baraza hilo Godfrey Mngereza
alisisitiza kwa mara nyingine tena kuwa hawajaifuta adhabu kwa Shilole
na sasa wanajipanga kumjadili tena baada ya kukiuka adhabu hiyo.
“Hakuna mahali ambapo panasema ameondelewa adhabu,” alisema.
“Kwa taratibu, baraza linaendeshwa kwa mujibu wa sheria na hii ni
sheria ya bunge namba 23 ya mwaka 1984 na kanuni zake za baraza ambazo
ni za mwaka 2015. Sasa kikitokea kitu kama hicho tunarudi tena kwa
utaratibu ule ule ambao ulikuwa umetumika katika kutoa adhabu ndio mfumo
huo huo tena ambao utatumika,” alisema.
Note: Only a member of this blog may post a comment.