September 20 2015 nakuwa miongoni mwa Watanzania walioziona taarifa
kupitia Whatsapp na mitandao mingine ya kijamii kwamba Umoja wa
makampuni ya mawasiliano Tanzania umetoa tamko la kupokea maagizo kutoka
tume ya taifa ya uchaguzi kwamba kuanzia October 24 2015 mpaka October
26 kampuni hizi ziondoe mfumo wa DATA kwa Wateja wake wote ili kuzuia
usambazwaji wa taarifa za kupotosha kuhusu uchaguzi mkuu.
Dakika chache baadae nikakutana na maneno ya January Makamba ambaye ni Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ambapo kupitia Twitter page yake ambayo ni Verified aliandika >>> ‘Taarifa
inayoenezwa mitandaoni kwamba mifumo ya data itazimwa tarehe 24-26
Oktoba si ya kweli. Jitihada za kuhamisha mijadala hazitafanikiwa‘
Kwenye sentensi ya pili akaandika >>> ‘Taarifa
hiyo ina tarehe 19.09.2014. Waliotengeneza hawakuwa waangalifu. Pia Bw.
Rene Meza, aliyesemekana kaiandika ameandoka nchini kitambo


Note: Only a member of this blog may post a comment.