KESHO
Jumapili, Yanga itaanza harakati zake za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu
Bara kwa kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam huku straika wake, Amissi Tambwe akitaka pia
kutetea rekodi yake.
Msimu uliopita Coastal Union yenye maskani yake Tanga ilifungwa mabao
8-0 na Yanga huku Tambwe raia wa Burundi akifunga mabao manne peke
yake, hivyo anachotaka ni kuendeleza rekodi hiyo.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Tambwe aliyekuwa
mfungaji bora wa ligi kuu msimu wa 2013/14, alisema amejipanga vizuri
kuhakikisha anaitungua Coastal na kuendeleza rekodi yake.
“Nashukuru Mungu nilifanya vizuri wakati ule, sasa nimejiandaa vizuri
kufanya tena kama vile nilivyofanya ili kutetea rekodi yangu, ujue
kufunga mabao manne katika mechi moja si jambo dogo.
“Najua kuna ushindani mkubwa kuanzia ndani ya timu hadi uwanjani
unapopambana na wapinzani wako lakini nimepania kufanya vizuri na
kuifikia rekodi yangu dhidi ya Coastal,” alisema Tambwe.
Msimu uliopita Tambwe alifunga mabao 14 huku mfungaji bora Simon
Msuva wa Yanga akifunga mabao 17.Alipokuwa mfungaji bora, Tambwe
alifunga mabao 19.
Saturday, September 12, 2015
TAMBWE Anasubiri Kuipiga Coastal Nne Zake!
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Filed Under:
SPORTS AND ENTERTAINMENTS
on Saturday, September 12, 2015

Note: Only a member of this blog may post a comment.