RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, amewakomalia wagombea urais Tanzania kuhakikisha wanaikumbuka michezo hasa soka pindi mmoja wao atakaposhinda nafasi hiyo.
Magufuli na Lowassa ndiyo wenye nguvu ya kisiasa kwa sasa na kuna uwezekano mkubwa mmoja wao akashinda kiti cha urais.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Malinzi alisema yeyote atakayeshinda nafasi ya rais anatakiwa kutoa kipaumbele kwa maendeleo ya soka ili kuifanya Tanzania itambe kimataifa.
“Niwaombe tu wagombea wa urais, Magufuli na Lowassa kama mmoja wao akifanikiwa kuingia madarakani basi asitusahau wanamichezo kwani tunahitaji viwanja vya soka kwani vilivyopo ni vichache,” alisema Malinzi.
“Hata kama wakishindwa kujenga vipya bali vile vilivyopo wavisimamie kwenye ukarabati kwani kama hilo likifanikiwa naamini michezo itapiga hatua nchini.”


Note: Only a member of this blog may post a comment.