Huenda jitihada za Ray C kukirejesha kiuno chake kisichokuwa na mfupa zimeanza kuzaa matunda!
Kwa muda mrefu muimbaji huyo amekuwa akijaribu kuupunguza unene wake
uliompoteza muonekano wake wa zamani uliompa sifa jukwaani na sasa picha
zake mpya zinaonesha mafanikio.
Muimbaji huyo ambaye jina lake halisi ni Rehema Chalamila, ameshare picha zake mpya kuonesha hatua aliyofikia.
“Haka ni kanani???yaani sitaki kuamini haka katoto ni mimi uwiii
!jamani nina furaha sana moyoni kumuona ray c.wa miaka ile yaani acha
tu!je nipungue zaid au?sasa ndio muda wa kurudi rasmi kwenye muziki
Babutale, Mkubwafela dada yenu niko tayari sasa,” ameandika.
Unamuonaje Ray C huyu mpya?
Note: Only a member of this blog may post a comment.