Tuesday, September 22, 2015

Anonymous

Panya Wamevamia Gereza, Kilichofuata Sasa ni Story....

Panya akiingia ndani ya nyumba na kuanza kusababisha uharibifu wake, hapo ndio ambapo unaanza kuonekana umuhimu wa kufuga paka.
Zaidi ya wafungwa 4,000 wamehamishwa kutoka ndani ya gereza la Pollsmoor lililopo Afrika Kusini baada ya panya kuvamia gereza hilo na kusababisha vifo vya wafungwa wawili.
ris
Mmoja wa viongozi wa gereza hilo Manelisi Wolela, amesema wamelazimika kuwahamisha wafungwa hao hadi pale watakapowaangamiza panya hao.
Amesema panya hao wamesababisha magonjwa kwa wafungwa na kuleta usumbufu mkubwa.
Gereza la Pollsmoor pia limeingia kwenye Historia ambapo Hayati Nelson Mandela aliwahi kufungwa katika gereza hilo wakati akiwa kwenye harakati za kutafuta Uhuru wa South Africa.

Tatizo ambalo limepelekea mpaka Wafungwa kufariki linatokana na magonjwa ambayo yanasababishwa na mkojo wa panya.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.