Tuesday, September 22, 2015

Anonymous

15 PICHAZ: Kutana na Jumba la Makumbusho Juu ya Milima! Italy na Rekodi Zao..


Juu ya Milima ya Kronplatz iliyoko Jimbo la South Tyrol, Italy.. hii ni moja ya vivutio vya aina yake kabisa, ni ubunifu wa Mhandisi Zaha Hadid.

Picha ya Juu ya Milima hiyo ndani ya Italy.
Juu ya Kilele cha Mlima Mkubwa Afrika ambao uko Tanzania, Mlima Kilimanjaro kuna theluji ambayo ni ya asili kabisa na ni kivutio kikubwa kinachofanya Watalii wengi wakitajiwa Mlima Kilimanjaro basi moja ya vitu vya kuvutia wanavyotamani kuviona ni ile theluji juu ya Mlima.

Pata picha unapanda juu ya Milima kutalii alafu unakutana na Mijengo ya Makumbusho ambayo ndani yake kuna vitu vingine pia vya kukuvutia uendelee kutalii.
 Nimezipata pichaz nje mpaka ndani ya Jumba la Makumbusho lililopewa jina la Messner Mountain Museum, kilichomo humo ni michoro ya kuvutia ambapo mbunifu wa Mjengo anasema hakuna kitu cha Sayansi wala maonesho ya sanaa ndani yake, ni michoro inayohusu masuala ya binadamu na Milima, basi !!





Hapa ni ndani tayari, baadhi ya watu wanaendelea kujionea vivutio vilivyomo humo.



Muonekano wa ndani, pichaz za michoro ya Milima ziko ukutani pamoja na vitu vingine vya kuvutia.


Huu ndio muonekano mwingine wa muundo wote wa Mjengo wenyewe nje mpaka ndani.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.