Nyota wa Taifa Stars, Shomari Kapombe.
Nicodemus Jonas
Dar es Salaam
MASTAA wa Nigeria, Antony Ujah anayekipiga Werder Bremen ya
Ligi Kuu Ujerumani ‘Bundesliga’ na Ahmed Mussa anayekipiga CSKA Moscow
ya Ligi Kuu Urusi, wamewataja nyota wa Taifa Stars, Shomari Kapombe na
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kama watu wenye viwango vya kucheza nje ya
nchi.
Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Licha ya ustaa wao, beki ya Stars ilifanikiwa kutuliza mashambilizi
ya mafowadi wa Nigeria, ikiongozwa na Emmanuel Emenike, Musa na Ujah
aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Emenike.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kuhusu viwango vya wachezaji wa Kitanzania, kila mmoja alikuwa na mtu wake.
Ujah alisema: “Kitu kikubwa Tanzania wanacheza kitimu ‘team work’,
hakuna aliyejua wangeweza kucheza soka zuri kiasi hiki lakini ndiyo
hivyo, tumepata pointi moja. Wengi wanacheza vizuri, lakini beki wa
kulia (Shomari Kapombe) anaweza kucheza ligi nje ya hapa.”
Kwa upande wa Mussa, alisema Cannavaro alikuwa mtu tegemeo kwa Stars katika mchezo huo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.