Boniphace Ngumije
Skendo! Mpangaji
aliyejitambulisha kwa jina la Mama Alex, mkazi wa Survey Mwenge, jijini
Dar, anadaiwa kutifuana na mama mwenye nyumba yake, Georgina Zamani kwa
madai ya ushirikina.
Mama mwenye nyumba, Georgina Zamani.
Habari kutoka nyumbani hapo zilidai
kwamba, kufuatia ishu hiyo, baba mwenye nyumba, Pius Zamani ameisusa
familia yake kutokana na madai hayo dhidi ya mkewe anayetuhumiwa kwa
ulozi.
Akizungumza na gazeti hili, Georgina
alisema matatizo kati yake na mumewe yalianza baada tu ya mpangaji huyo
kuhamia nyumbani kwake hapo miaka mitatu iliyopita.
Alidai kwamba, jambo lililomshangaza ni
jinsi mpangaji huyo anavyoishi kwenye nyumba hiyo bila kulipa kodi huku
mara kwa mara akimtuhumu kuwa yeye ni mchawi.
Georgina,
maarufu kwa jina la Mama Irene alisema kuwa, ilifika hatua mpangaji
huyo akawa anamtukuna hadharani, yeye na mwanaye Irene huku akisambaza
maneno kuwa ni mchawi.
“Nakumbuka ilikuwa Agosti 31 (mwaka
huu), mpangaji huyo alianza kumtukana mwanangu akidai kuwa tumechukua
nguo zake na kuzikata kila moja kwenye pindo, jambo lililonifanya
nimfuate kumuuliza, lakini nilipomsogelea tu mume wangu akaja na kuanza
kumpiga Irene akidai ni kweli tulifanya hivyo.
“Baada ya tukio hilo, mume wangu akawa
hanisemeshi, hatoi fedha ya matumizi na wala halali chumbani kwangu.
Akawa anakula kwa mpangaji huyo kisha analala chumba cha wageni.
Mjumbe wa nyumba kumi, Kuruthumu Bakari.
“Nilitoa taarifa kwa mjumbe wa nyumba
kumi (Kuruthumu Bakari) lakini aliniambia nilipeleke shauri langu kwenye
Baraza la serikali za mitaa,” alisema mama mwenye nyumba.
Kwa upande wake Mama Alex alikanusha
madai ya kuishi bila kulipa kodi (japo hana mkataba) pamoja na kuchepuka
na mume wa Georgina, akaongeza kuwa kinachomsumbua mahali hapo ni
vitendo vya kichawi anavyokuwa anafanyiwa, kikiwemo hicho cha kanga zake
kukatwa vipande kwenye pindo.
Alipoulizwa kwa nini asihame, mama Alex
alifunguka: “Siwezi kuhama kwa sababu sina tatizo na baba mwenye nyumba,
nitatoka fedha yangu itakapoisha.”
Baadhi ya majirani wa Georgina walisema kuwa, Mama Alex ni mshari na amekuwa akitifuana na mama mwenye nyumba mara kwa mara.
Juhudi za kumtafuta baba mwenye nyumba na mume wa mpangaji huyo kuzungumzia jambo hilo hazikuzaa matunda.

Note: Only a member of this blog may post a comment.