Yamoto Band inawatahadharisha watanzania kuhusu utapeli uliozuka mtandaoni wa kuomba rambirambi za msiba wa mama yake na Aslay
“Kuna mtu anatumia akaunti feki ya msanii wa Yamoto Band, Enock Bella
akiomba kutumiwa rambirambi ya msiba wa mama mzazi wa Aslay Isihaka
ambaye amefariki dunia leo asubuhi,” mtu aliye karibu na bendi hiyo
ameiambia Bongo5.
“Mtu huyo anatumia namba 0716281999 na amesajili kwa jina la Aslay
Isihaka. Tunawaomba wadau na mashabiki wa Yamoto Band na Aslay wapuuze
tarifa hiyo sio za ukweli na hakuna utaratibu wa kutuma rambirambi
katika simu.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.