Jux amedai kuwa Jackie Cliff (aliyekuwa girlfriend wake) aliyedaiwa
kukamatwa na madawa ya kulevya nchini China na kufungwa jela,
anaendelea vizuri na anafuatilia kila kitu kinachoendelea Bongo.
Jux amesema Jackie anajua mahusiano yake na Vanessa Mdee.
“Yeah tunawasiliana tunaongea,” amesema Jux. “Anajua kila kitu
kinachoendelea. Tunaongea vizuri, yuko poa kabisa na habari za Bongo
kila kitu anajua yaani,” Jux alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha
East Africa TV.
“Kuna habari nyingine hata mimi nashangaa anajuaje, kwa sababu kuna
rafiki zake wengine wanaenda kumuona, pia mimi ni kijana I want to move
on in my life, na yeye mwenyewe anajua inabidi niendelee na maisha,
kikubwa zaidi tunawasiliana na hatuna mahusiano yoyote mabaya.”
Note: Only a member of this blog may post a comment.