Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema serikali yake
haitamshtaki askari polisi ikiwa ataua jambazi mwenye silaha.
“Katika serikali yangu askari akimpiga jambazi mwenye silaha kwa risasi
hashtakiwi. Kila mara (majambazi) wanavamia vituo vya polisi, mbona
hawavamii kambi za jeshi, Jeshi la Kujenga Taifa au Ukonga FFU?, wanaona
polisi wana nidhamu sasa wanawaonea na kuwaua,” alisema Magufuli.
Mgombea huyo wa urais wa CCM pia aliahidi kwamba ataboresha maslahi ya
askari polisi ili wafanye kazi zao kwa ufanisi na wakiwa na furaha.
Kadhalika, aliahidi kuwa akichaguliwa kuwa Rais, atahakikisha makusanyo
ya kodi kwa mwezi yanaongezeka mara mbili kutoka yanayokusanywa sasa ya
Sh. bilioni 900 hadi Sh. tirioni 1.8.


Note: Only a member of this blog may post a comment.