Klabu ya soka ya Sporting Lisbon ya nchini Ureno, imemsainisha kijana
aliyenusurika kifo kwenye tetemeko wimbi la tsunami nchini Indonesia,
Martunis kwenye academy yao, ikiwa ni miaka 11 baada ya janga hilo
lililomfanya aokoe maisha yake kwa kukaa kwenye dimbwi la maji kwa siku
21 huku mama yake na kaka zake wawili wakipoteza maisha.
Martunis, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 17, alitangazwa kwenye
mji mkuu wa Ureno, Lisbon baada ya kuwa na ndoto ya kucheza soka la
kulipwa, licha ya uharibifu mkubwa uliofanywa na mafuriko hayo nchini
Indonesia, December 26, 2004.
Kijana huyo ameingizwa kwenye academy ya Sporting na msimu ujao anaweza kucheza kwenye timu ya wachezaji walio chini ya miaka 19
Mafuriko/mawimbi hayo makubwa yalisabibishwa na tetemeko la ardhi kwenye bahari ya Hindi na kuua watu 230,000 katika nchi 14.
Sasa Martunis ameungana na chuo hicho maarufu cha Sporting
kilichokikuza kipaji cha mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na
Luis Figo.
‘Ni jambo kubwa kuwa hapa, klabu hii inaifanya ndoto yangu
iwezekane,” alisema kijana huyo. “Nimefurahi mno kwa fursa hii. Viva
Sporting.”
Ronaldo alikutana na Martunis baada ya janga hilo baada ya picha zake
akiwa na jezi ya Ureno aliyokuwa ameivaa wakati wa akicheza mpira muda
ambao tetemeko hilo lilitokeo ziliposambaa mtandaoni.
Martunis alikuja kuonana na baba yake lakini mama na kaka zake wawili
walikuwa miongoni mwa watu waliopoteza maisha kwenye janga hilo kubwa
la asili kuwahi kutokea duniani.
Nyumba ya mtoto huyo aliyekuwa na miaka saba ilijengwa kwa kutumia
fedha zilizotumwa na chama cha soka cha Ureno na kukusanywa kwa jitihada
za Ronaldo za kuchangisha fedha.
Ronaldo na mtoto huyo walikuja kukutana miaka mitatu baadaye.
Ronaldo aliyeanza kuchezea soka kwenye club hiyo aligharamikia elimu yake.

Note: Only a member of this blog may post a comment.