Pichani:kulia ni Mkurugenzi wa huduma za kisheria wa tume ya Uchaguzi, Emmanuel Kawishe.
Tukiwa bado tupo kwenye headlines za
Uchaguzi 2015 hivi karibuni kumekuwa na taarifa zilizoenea kuhusu vijana
waliopatikana katika mikoa kadhaa kusimamia kura au masanduku ya
Uchaguzi Mkuu 2015 katika kila jimbo.
Sasa leo Sept 29,2015 ripota wa
Amplifaya alikutana na Mkurugenzi wa huduma za
kisheria wa tume ya Uchaguzi, Emmanuel Kawishe kupata majibu sahihi
kuhusiana na taarifa hizo..’Hakuna watu
walioteuliwa kwenda kusimamia masanduku na tume itaanza rasmi kuwateuwa
kuanzia tarehe 26 mwezi wa tisa sasa hivi tume imeanza mafunzo mpaka
tarehe 3 mwezi wa kumi tunatoa mafunzo kwa usimamizi wa uchaguzi ngazi
ya jimbo na wasaidizi wao tutaenda kwenye kata pia tutaenda kwenye
vituo kwa hiyo hao ndio tume itatoa mafunzo kwao – Emmanuel Kawishe
‘Sheria
inakataza kwamba haruhusiwa mtu yoyote kupiga kampeni siku ya uchaguzi
wala haruhusiwa mtu kuja na nguo ya chama chochote katika chumba cha
kupigia kura kwa hiyo wewe njoo na nguo za kawaida na kadi yako ya
kupigia kura basi wasimamizi watakupa maelekezo ya kila kitu‘ – Emmanuel Kawishe
Bonyeza play au download kusikiliza mahojiano hayo live
Bonyeza play au download kusikiliza mahojiano hayo live
Note: Only a member of this blog may post a comment.