Friday, September 4, 2015

Anonymous

Je, Mahakama ya Kimataifa ya ICC Kusimamia uchaguzi 2015? Majibu Yako Hapa

Tukiwa bado kwenye headlines za Uchaguzi 2015 kuna taarifa ambazo zilikuwa zinasambaa hivi karibuni kwamba Mahakama ya kimataifa ya ICC itakuja Tanzania kusimamia Uchaguzi.
Sasa leo ripota wetu alikutana na Mkurugenzi wa huduma za kisheria wa tume ya Uchaguzi, Emmanuel Kawishe kupata majibu sahihi kuhusiana na taarifa hizo..

‘Kawaida taasisi ili ije kutazama uchaguzi lazima itume barua ya maombi lakini kwa ICC bado hawajaomba na kuna category  za taasisi  zinataka kuomba kwa hiyo kama itaangukia kwenye sifa basi tutaruhusu lakini kama hiyo taasisi haina sifa haturuhusu, kwa sasa tumepokea taasisi za kimataifa kama 20 na za hapa ndani ni zaidi ya 60’ – Emmanuel Kawishe 

‘Kwa hiyo tunaendelea kupokea na tunaendelea kuangalia taasisi zingine zinakosa vigezo tunawaambia taasisi zenu hazijakizi vigezo nendeni halafu mrudi tena kwa hiyo wale wanaokizi vigezo tunawapokea‘ – Emmanuel Kawishe
Sikiliza live hapo chini kwa kubonyeza play au download!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.