Beyonce katika pozi na Jay Z.
New York, MarekaniRAPA mwenye heshima ya muda wote kwenye gemu la Hip hop duniani, kutoka Marekani Shown Carter ‘Jay z’ hivi karibuni alimfanyia ‘surprise’ mkewe, Beyoncé Giselle Knowles-Carter kwenye sherehe ya kuazimisha miaka 34 tangu azaliwe, kwa kumchagulia wimbo wa kuisindikiza furaha yake ambao hakuutegea kabisa.
Beyonce akiwa na mwanaye Blue Ivy.
Akizungumza na mtandao maarufu Marekani baada ya sherehe hiyo
iliyofanyika Septemba 4, Beyonce ambaye ni mama wa mtoto mmoja Blue Ivy
alisema, amemzoea mumewe kuwa ni mpenzi sana wa muziki wa Hip hop lakini
kitendo chake cha ‘kumdediketia’ wimbo wa Yellow wenye mahadhi ya Rock
ukiimbwa na Coldplay kilimuacha hoi sana.“Nimeufurahia sana wimbo alionichagulia Jay Z, siyo siri kwangu ilikuwa ni surprise kubwa ambayo naamini ameifanya kwa sababu ananipenda, nichukue nafasi hii kuwashukuru watu wote walionipa sapoti kwa kufika kwenye siku hii muhimu kwangu,” alimaliza Beyonce.

Note: Only a member of this blog may post a comment.